top of page

Ashikiliwa na polisi kwa kufanya biashara ya viungo vya binadamu.

  • Writer: Arbostar
    Arbostar
  • Jan 6, 2018
  • 1 min read

Mtuhumiwa huyo aliyejulikana kwa jina la Moshe Harel, anashikiliwa na jeshi la polisi nchini Cyprus kwa tuhuma za kufanya biashara ya figo kwa matariji wa Israel takriban miaka kumi sasa.


Amehusishwa kuchukua figo za raia wa Kosovo pamoja na Uturuki na nchi nyingine kadhaa ambao mpaka sasa hajawalipa chochote.


Mnamo mwezi December mtu huyo alikamatwa uwanja wa ndege wa Larnaca kwa maelezo ya msemaji wa jeshi la polisi la Cyprus.


siku ya Jumanne Anatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayomkabili.


Nchini Kosovo anahitajika kwa makosa kama hayo pia.


Source: http://www.bbc.com/swahili/habari-42590925

Moshe Harel anatajwa kuwa na ushirikiano wa karibu na wafanya biashara wakubwa wa viungo vya binadam


Comments


bottom of page